Hamtafikia Kabisa Wema Mpaka Mtoe Katika Vile Mnavyovipenda!

 Anasema Allaah (سبحانه وتعالى)

((لَنْ تَنَالُواْ الْبِرَّ حَتَّى تُنفِقُواْ مِمَّا تُحِبُّونَ وَمَا تُنفِقُواْ مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللّهَ بِهِ عَلِيمٌ))

 

((Hamtafikia kabisa wema hadi mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachokitoa basi hakika Allaah Anakijua)) [Al-'Imraan 3: 92]

 

Katika kutoa sadaka anatakiwa Muumini atoe katika vile vilivyokuwa ni vizuri na bora kabisa hapo ndipo atakapokuwa kafikia wema kama inavyotaja kauli hiyo ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Kisha cha Abu Twalhah na bustani yake kipenzi Al-Bayruhaa:

 

عن أنس بن مالك يقول: كان أبو طلحة أكثر أنصاري بالمدينة مالا وكانَ أحبَّ أمواله إليه بيْرَحاءُ  , وكانت مُسْتقْبلة المسجد، وكان النبي صلى الله عليه وسلم يدخلها ويشرب من ماء فيها طيّب , قال أنس: فلما نزلت: ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) قال أبو طلحة: يا رسول الله، إن الله يقول: ( لَنْ تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّى تُنْفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ) وإن أحبَّ أموالي إلَيَّ بيْرَحاءُ وإنها صدقة لله أرجو بِرَّها وذُخْرَها عند الله تعالى، فَضَعْها يا رسول الله حيث أراك الله [تعالى]  فقال النبي صلى الله عليه وسلم: ((بَخٍ، ذَاكَ مَالٌ رَابِحٌ، ذَاكَ مَالٌ رَابِح، وَقَدْ سَمِعْتُ، وَأَنَا أرَى أنْ تجْعَلَهَا فِي الأقْرَبِينَ)). فقال أبو طلحة: أفْعَلُ يا رسول الله. فَقَسَمها أبو طلحة في أقاربه وبني عمه (رواه  أحمد )

 

Imetoka kwa Anas bin Maalik رضي الله عنه kwamba Abu Twalhah alikuwa na mali kuliko yeyote miongoni mwa Answaar wa Madiynah na kilichokuwa kipenzi kabisa katika mali yake ni bustani ya Bayruhaa ambayo ilikuwa mbele ya msikiti wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم .  Mara nyingine Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alikuwa akienda katika bustani hiyo na kunywa maji yake baridi. Anas akaongeza kusema: Aayah hii ilipoteremka (Hamtafikia kabisa  wema  mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda) Abu Twalhah akasema "Ewe mjumbe wa Allaah, Allaah Anasema, (Hamtafikia kabisa  wema   mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda) bila ya shaka bustani ya Bayruhaa ni kipenzi katika mali zangu. Kwa hiyo nataka kuitoa sadaka kwa ajili ya Allaah nikitegemea thawabu zake na malimbikizo kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى . Ewe mjumbe wa Allaah, itumie popote Anapokuonyesha Allaah kuwa ni bora kuitumia". Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Umefanya vizuri, Ni mali yenye faida, ni mali yenye faida.  Nimesikia ulivyosema na nafikiri itakuwa ni bora kuwapa walio karibu yako [jamaa zako])) Abu Twalhah akasema "Nitafanya hivyo ewe Mjumbe wa Allaah". Abu Twalha akagawa kwa jamaa zake na watoto wa ami yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim, Ahmad]

 

Hawa ndio Maswahaba walioamini kweli na kusabilia mali zao katika njia ya Allaah bila ya kujali lolote.  

 

Naye 'Umar bnul Khattwaab رضي الله عنه alitoa mali yake iliyo kipenzi kabisa.

 

عُمَر  رضي الله عنه   قال :  " يا رسول الله، لم أُصِبْ مالا قطُّ هو أنْفَسُ   عندي من سهمي الذي هو بِخَيْبَرَ، فما تأمرني به؟"   قال : ((حَبِّس الأصْل وسَبِّل الثَّمَرَةَ))  مسلم والنسائي من إبن ماجاه

 

‘Umar رضي الله عنه alisema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, Sijapata kumiliki kipande cha mali kilicho cha thamani kwangu kama sehemu yangu ya Khaybar. Kwa hiyo unaniamuru niifanye nini?"  Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Ibakishe ardhi  na utoe mazao yake kwa ajili ya Allaah [Fiy Sabili-Llah]))   [Muslim na An-Nasaaiy kutoka kwa Ibn Maajah]

 

Na kutoa sadaka ni kama mkopo wa kumkopesha Allaah سبحانه وتعالى . Hili ni jambo  kubwa, zuri, lenye kuzidisha iymani zetu na lenye kustaajabisha vilevile, kwa kuwa Mola wetu Mtukufu Ndiye Anayemjaalia mja Wake kumpa mali, kisha Yeye Anatuambia tumkopeshe hiyo mali na kuwa Atatulipa zaidi kuliko hiyo tutakayoitoa kwa ajili Yake! Na Juu ya yote, Atatupa malipo ya ukarimu! Subhana Allaah! Ukarimu ulioje wa Mola Mtukufu! Kama anavyosema:

 

((مَن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ وَلَهُ أَجْرٌ كَرِيمٌ))

 

((Ni nani atakayemkopesha Allaah mkopo mwema, ili Amrudishie maradufu, na apate malipo ya ukarimu)) [Al-Hadiyd 57: 11]

 

 Na tutambue kwamba chochote utoacho ndugu  Muislamu ikiwa kikubwa au kidogo mno vipi basi Allaah (سبحانه وتعالى) Haghafilika nacho bali Atakulipa malipo yake duniani kama Anvyotuambia Allaah (سبحانه وتعالى) :

 

))وَمَا تُنفِقُونَ إِلاَّ ابْتِغَاء وَجْهِ اللّهِ وَمَا تُنفِقُواْ مِنْ خَيْرٍ يُوَفَّ إِلَيْكُمْ وَأَنتُمْ لاَ تُظْلَمُونَ((

((Na chochote mtoacho iwe ni kwa kutafuta radhi za Allah, na chochote mtoacho cha kheri mtalipwa kikamilifu nanyi hamtadhulumiwa)) [Al-Baqarah 2: 272]

Pia Anasema Allaah (سبحانه وتعالى)

 

((وَأَقْرِضُوا اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا))

 

((..na mkopesheni Allaah mkopo mwema. Na kheri yoyote mnayoitanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Allaah, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana..)) [Al-Muzzmmil: 73: 20]

 

 

************

0 Comments