Katibu Mkuu wa UN aikosoa serikali ya India kwa ubaguzi inaowafanyia Waislamu wa nchi hiyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameikosoa serikali ya India kwa ubaguzi inaowafanyia Waislamu wa nchi hiyo.

Katika ujumbe maalumu aliotoa, Guterres amesema: Wakati viongozi wa chama tawala cha Wahindu nchini India wanajaribu kuonyesha kuwa Waislamu ndio waliosababisha kuenea virusi vya corona nchini humo, tunashuhudia jinsi Waislamu hao wanavyoandamwa na hujuma za kibaguzi na kushindwa kupata huduma zinazohitajika kwa ajili ya kukabiliana na virusi vya corona.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita zimeshuhudiwa hatua na maamuzi kadhaa yaliyochukuliwa na serikali ya India dhidi ya Waislamu, ambayo yamezusha malalamiko makubwa nchini humo.


Kuwapatia Wahindu ardhi ya msikiti wa kihistoria waliubomoa wa Babri, kufutwa mamlaka maalumu ya ndani ya kujiendeshea mambo yake liliyokuwa limepewa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India ambalo wakazi wake ni Waislamu, kubatilishwa uraia wa mamia ya maelfu ya Waislamu, kupitishwa sheria mpya ya uraia na kuwapatia uraia wa India raia wa kigeni kwa sharti la kutokuwa Waislamu, ni baadhi tu ya maamuzi ya kibaguzi yaliyochukuliwa na serikali ya chama tawala cha Kihindu cha Bharatiya Janata (BJP) nchini India dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo.

0 Comments