Kiongozi wa Ikhanul Muslimin afia jela Misri baada ya kunyimwa huduma za matibabu

 

Mmoja kati ya viongozi wa harakati kubwa zaidi ya upinzani dhidi ya seriikali ya Misri ya Ikwanul Muslimi ameaga dunia kiwa jela kutokana na matatizo ya moyo.


Televisheni ya al Jazeera ya Qatar imeripoti kuwa, Issam al Aryan aliaga dunia jana Alkhamisi katika jela ya kutisha ya Tora ya Cairo kutokana na matatizo ya moyo.


Wakili wa afisa huyo mkubwa wa Ikhwanul Muslimin Abdel Moneim Abdel-Maqsoud amesema kuwa, jana uongozi wa jela hiyo ulimtaarifu kwamba al Aryan ameaga dunian ndani ya jela ya Tora.


Wakili Abdel-Maqsoud amesema Isam al Aryan alizuiwa kukutana na familia yake kwa zaidi ya miezi sita iliyopita kwa kisingizio cha maambukizi ya virusi vya corona.


Wakati wa kikao cha kusikiliza kesi yake, kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Ikhwanul Muslimin alikuwa amelalamika kwamba, ananyimwa huduma ya matibabu na kutelekezwa.


Al Aryan alitiwa nguvuni mwaka 2013 baada ya mapinduzi ya jeshi yaliyoongozwa na jenerali Abel Fattah al Sisi dhidi ya serikali ya kwanza kuchaguluwa kidemokrasia nchini Misri ya Muhammad Morsi.


Al Aryan ni miongoni mwa viongozi wa Ikhwanul Muslimin waliokuwa wamekuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa tuhuma kadhaa zinazohusiana na masuala ya kiusalama.


Al Aryan anajiunga na viongozi na mamia ya wanaharakati wa upinzani nchini Misri walioaga dunia wakiwa jela kutokana na kunyimwa huduma za matibabu na kutelekezwa.  


Rais wa zamani wa nchi hiyo Mohammad Morsi pia alianguka chini na kufariki dunia akiwa kwenye chumba cha mahakama tarehe 17 Juni mwaka jana nchini Misri.  


Wakati huo mashirika ya kutetea haki za binadamu yalisema: Mauaji yanayofanyika kwa kunyimwa huduma za tiba ndani ya jela na mahabusu za Misri yangali yanaendelea na yanachukua roho za wafungwa wa kisiasa kwa mpangilo na mfumo maalumu.

0 Comments