Shaykh Swaalih Bin Muhammad Al-Luhaydaan

 Ni ‘Aalim mkubwa na Daa’iy (mlinganizi) wa kuheshimiwa; Swaalih bin Muhammad Al-Luhaydaan.

 

Alizaliwa katika mji wa Al-Bukayriyyah katika mtaa wa Qasiym nchini Saudi Arabia katika 1350 BH (baada ya Hijrah).

 

 

Alimaliza masomo yake katika kitivo cha Shariy´ah mwaka wa 1379 B.H na akafanya kazi kama katibu wa Shaykh Muhammad bin Ibraahiym Aal-Shaykh ambaye alikuwa ni Muftiy wa Saudi Arabia mpaka katika mwaka wa 1383 B.H alipokuwa msaidizi wa mkuu katika mahakama ya juu Riyadh. Katika mwaka wa 1384 B.H alikuwa mwenyewe mkuu wa mahakama.

 

 

Alipata shahada yake ya pili kutoka katika Chuo kikuu cha u-Qaadhiy katika mwaka 1389 B.H na aliendelea kuwa kiongozi wa hayo mahakama kuu mpaka mwaka wa 1390 B.H.  Kwa hivyo akawa jaji wa mahakama ya rufaa na mjumbe wa baraza la mahakama kuu ya u-Qaadhiy.

 

 

Katika mwaka wa 1402 B.H akawa mkuu wa baraza la mahakama ya kudumu, na makamu wa mkuu wa Bunge la hukumu. Katika mwaka wa 1413 B.H akawa mkuu wa bunge la hukumu.

 

 

Ni mjumbe wa baraza la ‘Ulamaa wakubwa (Kibaar Al-´Ulamaa) kuanzia mwaka wa 1391 B.H na ni mjumbe wa Raabitwat-ul-'Aalam Al-Islaamiy.

 

Alikuwa pia na juhudi za kuanzisha gazeti la Raayat-ul-Islaam, na akawa mhariri na mwenyekiti wake.

 

Amefundisha pia katika Msikiti mkuu mjini Makkah na ametoa Fataawa katika redio ya kipindi cha Nuwr 'alaa Ad-Darb. Huwa akitoa hali kadhalika mihadhara na kushiriki katika makongamano mbalimbali.

 

Ameshajiisha pia elimu na watu kuendelea kusoma shahada ya pili na shahada ya udaktari (PHD) na mambo mengine yenye faida.

 

 

Chanzo: Ad-Durar as-Saniyyah 16/489.

0 Comments