September 23, 2020

Benki ya Jaiz ya Nigeria yapata zawadi ya benki bora ya Kiislamu


Tuzo ya Kimataifa ya Mfumo wa Kifedha wa Kiislamu (GIFA) imetoa  zawadi hiyo kwa Benki ya Jaiz na kusema benki hiyo imechaguliwa kutokana na kuimarisha shughuli zake za kutoa huduma kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu. Mbali na kutambuliwa kutokana na kuzingatia sheria za Kiislamu katika huduma zake, benki hiyo pia imetambuliwa kutokana na jitihada za kuimarisha maisha ya wafanyakazi wake na jamii kwa ujumla. Mkurugenzi wa GIFA, Profesa Humayoun Dar amemuandikia barua Mkurugenzi Mkuuwa Benki ya Jaiz Hassan Usman na kupongeza kwa mafanikio hayo.

Kwa upande wake, Usman ametoa shukrani zake zake kwa GIFA kutokana na zawadi hiyo ambayo ni ishara ya wazi kuwa juhudi za benki hiyo zinatambuliwa kimataifa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only