September 19, 2020

Mwanamke Muislamu Marekani aishtaki polisi kwa kumvua Hijabu

 Mwanamke Muislamu nchini Marekani amewasilisha kesi mahakamani na kusema haki zake za kiraia na kidini zilikiukwa pale maafisa wa Idara ya Polisi ya Los Angeles (LAPD) walipomvua Hijabu (mtandio) wakati akihudhuria mkutano wa Tume ya Polisi mwaka jana.Nusaiba Mubarak, 26,  alikuwa anasubiri kutoa ushahidi kuhusu ukatili wa maafisa wa LAPD, wakati maafisa watatu wa polisi walipomuhujumu ghafla, kumuweka pingu na kumuingiza katika chumba kingine ambapo walimvua mtandio wake na kumdhalilisha.


Mubarak ambaye anawakilishwa na mawakili wa Baraza la Marekani la Mahusiano ya Kiislamu (CAIR), amesema kitendo cha maafisa wanaume kumvua Hijabu hni ukiukwaji wa mafundisho ya Kiislamu. Aidha amesema  kukamatwa kwake kulikuwa kinyume cha sharia kwani hakuwa amefanya kosa lolote. Aidha anasema aliachiliwa pasina kufunguliwa mashtaka na kuongeza kuwa tukio hilo lilimshtua sana.


Bi. Mubarak anasema alikuwa amehudhuria kikao cha Tume ya Polisi Septemba mwaka jana  kulaani mauaji ya Albert Ramon Dorse, ambayo alipigwa risasi na kuuawa na afisa wa LAPD mnamo Oktoba 2018. Baada ya kukamatwa na kuvuliwa Hijabu, Bi. Mubarak hakuweza kutoa ushahidi katika tume hiyo. 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only