October 5, 2020

Al-Azhar yalaani kauli ya Rais Macron wa Ufaransa dhidi ya Uislamu

 


Baraza la Utafiti wa Kiislamu la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar cha nchini Misri  limesema katika taarifa yake kwamba, madai ya Rais Macron kuhusu Uislamu ni batili na katu hayana uhusiano wowote na Uislamu.


Sehemu moja ya taarifa hiyo ya Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar cha nchini Misri imesema: Tunapinga na kulaani vikali matamshi haya na tunasisitiza kwamba, matamashi haya ni ya kibaguzi na yamejeruhi hisia za Waislamu bilioni moja ulimwenguni.


Kadhalika Baraza la Uhakiki wa kiislamu la Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar  limelaani hatua ya baadhi ya watu ya kung'ang'ani kuutuhumu Uislamu na dini nyingine kwa tuhuma zisizo na msingi wowote.


Aidha Sheikh Ahmad Tayyib, Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar cha Misri naye ametangaza wazi upinzani wake dhidi ya matamshi hayo ya Rais wa Ufaransa aliyetumia neno la ugaidi wa Kiislamu.


Katika mwendelezo wa sera za kupiga vita Uislamu nchini Ufaransa, Emmanuel Macron juzi alizindua mpango wa kulinda thamani za kisekulari za nchi hiyo dhidi ya kile kilichotajwa kama "Misimamo Mikali ya Kiislamu". Rais wa Ufaransa alidai kuwa Uislamu ni dini iliyo "kwenye mgogoro" ulimwengu mzima.


Katika hotuba yake hiyo ambayo imewaudhi Waislamuwa maeneo mbalimbali ulimwenguni Macron alisema, serikali yake itawasilisha muswada mwezi Desemba wa kuimarisha sheria ya 1905 ya nchi hiyo ambayo ilitenganisha rasmi Kanisa na utawala.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only