Kukata Kucha Siku Ya Ijumaa

 SWALI:

Why did Mtume Muhamad SAW used to cut his nails on Friday. What was the reason for cutting his nails on Fridays. Please advise

 


 


JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

Kujisafisha siku ya Ijumaa kwa kukoga (Ghuslu), kukata  kucha,  kuvaa nguo iliyo nzuri kabisa na kujitia manukato (kwa wanaume) ni katika kuiadhimisha siku hii tukufu ya Ijumaa kwani kufanya hivyo ni kufuata amri ya Allaah سبحانه وتعالى   katika Qur'aan Anavyosema:

 ذَلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ حُرُمَاتِ اللَّهِ فَهُوَ خَيْرٌ لَّهُ عِندَ رَبِّهِ

 

Na anaye vitukuza vitakatifu vya Allaah basi hayo ndiyo kheri yake mbele ya Mola wake.  Hajj : 22:30

ذَلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ

Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allaah, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo Hajj 22:32


Ama Swali kuhusu sababu hasa inayohusu kukata kucha, ni kwamba ni mojawapo ya Sunnah ya Fitrah (Maumbile ya asili 'Pure Nature of Creation')  kama Aliyvosema Allaah سبحانه وتعالى  

 فِطْرَةَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا

ndilo umbile la Allaah Alilo waumbia watu Ar-Ruum:30

Na Sunnah hii ya Fitrah imesisitizwa katika Hadithi mbali mbali.  Sunnah ambayo inapotimizwa huleta maslaha pande mbili ambazo ni:

          1)    Siha ya binaadamu

          2)    Kutimiza amri za dini

Kutokana na pande zote mbili hizo, faida zinazopatikana ni;

·         Kuepukana na maradhi.

·         Kudhihirisha uzuri na usafi.

·         Kuitukuza na kuiridhisha  nafsi (kuwa imetimiza Sunnah).

·         Kutimiza Twahara ya wudhuu vizuri.

·         Kuukirimu ubinaadamu. 

Hadithi ifuatayo inatufundisha vitu vya kufanya katika mwili wetu kupatikana Fitrah:

عن أبي هريرة رضي الله عنه، عن النبي   قال: )) الفطرة خمسة، أو خمس من الفطرة . الختان، والاستحداد، وتقليم الأظفار، ونتف الإبط، وقص الشارب (( متفق عليه

Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kasema; ((Fitrah ni tano, au (vitu) vitano miongoni ni mwa Fitrah, Kutahiri (Circumcision), kunyoa (au kupunguza ) nywele za sehemu ya siri (pubic hair),  kukata kucha, kunyofoa (au kunyoa) nywele za kwapani, na kupunguza  mashurubu))  Al-Bukhari na Muslim  

Na kufanya hayo tumewekewa muda wa siku Arubaini  tusipitize bila kukamilisha Fitrah hiyo.

 عن أنس بن مالك رضي الله عنه، قال. " وقت لنا - وفي رواية، قال: وقت لنا رسول الله   في قص الشارب وتقليم الأظافر ونتف الإبط وحلق العانة. أن لا نترك أكثر من أربعين ليلة  أخرجه أبو داود والترمذي ومسلم والنسائي. وقال أبو داود: " وقت لنا " أصحوقال النسائي: وأكثر من أربعين يوما "، وقال مرة " أربعين ليلة"  

Imetoka kwa Anas bin Maalik  رضي الله عنه ambaye alisema; Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  alituwekea muda wa kupunguza masharubu, kukata kucha, kunyofoa (au kunyoa) nywele za kwapa, na kunyoa (au kupunguza) nywele za sehemu za siri (pubic hair), kwamba tusiziache zaidi ya siku Arubaini. Muslim, Abu Dawuud, At-Tirmidhiy na An-Nasai

Kuhusu kukata kucha Ijumaa kumependezewa kwa sababu Muislam anatakiwa siku ya Ijumaa ajisafishe na kujipamba wakati anakwenda msikitini, na hivyo basi kukata kucha ni jambo moja katika usafi huo.  

Vile vile kukata kucha siku ya Ijumaa pamoja na kupunguza masharubu na kunyoa au kupunguza nywele za sehemu za siri (pubic hair), kunyofoa au kunyoa nywele za kwapa, na pia kujipaka manukato kwa mwanaume, kupaka mafuta nywele na ndevu zake na kuzichana, ni jambo lenye kupendeza kwa Muislam.

Vile vile, kucha zinapokuwa ndefu, wudhuu wa Swalah huwa ni vigumu kutekelezeka kikamilifu kwa uwezekano wa maji kutofika sehemu za ndani ya kucha. Vilevile kama mtu hajakuwa makini kwa usafi, kucha ndefu huhifadhi uchafu mara kwa mara.

Na Allaah Anajua zaidi

0 Comments