October 5, 2020

Ni jukumu la kila Muislamu kuilinda Yerusalemu

 


Rais Recep Tayyip Erdoğan amesema kuwa ni jukumu la kila Muislamu kuilinda Yerusalemu.

Rais Erdoğan, katika ujumbe aliomtumia Rais İshak Sağlam, kiongozi wa Kongamano la Kimataifa la Saladin Ayyub lililoandaliwa na (chama cha siasa) Hüda Par, alisema kuwa anamkumbuka mshindi wa pili wa Yerusalemu Saladin Ayyub na askari wake mashujaa.

"Saladin alijiuliza," Je! Saladin analalaje nyumbani kwake wakati nyumba ya Mwenyezi Mungu iko kifungoni. ' Alikuwa kamanda aliyeipenda sana Yerusalemu. " alikumbushia Erdoğan.

Mtunzi wa nyimbo wa Uturuki Mehmet Akif Ersoy katika wimbo wake wa "Sultan anayependwa zaidi " alielezea kwamba daima Saladin Ayyub amekuwa na nafasi tofauti sio tu katika mioyo ya Waislamu, lakini pia mbele ya wapinzani wake kwa haki yake,ujasiri, huruma na ushujaa.

"Saladin Ayyub alituokoa kutoka kwa uvamizi wa Crusader na kuifanya Yerusalemu kuwa mahali pa kuaminiwa tena kwa imani zote."

Akisisitiza kwamba ni jukumu la kila Muislamu kuilinda Yerusalemu, Erdoğan, ameongeza kwa kusema kuwa,

"Jaribio lolote ambalo linahalalisha uvamizi wa Israel, linakubali mipango ya Israel ya kutenganishwa kwa ardhi ya Yerusalemu na Palestina, na kupuuza haki halali za ndugu zetu Wapalestina, ni usaliti kwa imani ya Saladin."

Erdogan amesema kwamba kongamano hilo, limefanyika wakati ambapo juhudi kama hizo zilikuwa zinaongezeka chini ya hatua za "kuhalalisha" (makubaliano ya kuihalalisha Israel yalitiwa saini na Falme za Kiarabu na Bahrain katika Ikulu ya White House).

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only