October 26, 2020

Pogba 'ajiuzulu' timu ya taifa ya Ufaransa kufuatia matamshi ya Macron dhidi ya Uislamu


Mchezaji nyota wa soka, Paul Pogba ameripotiwa kujiuzulu katika timu ya taifa ya soka ya Ufaransa, kutokana na matamshi yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo ya Ulaya dhidi ya Uislamu, wakati akitetea vitendo vya kutusiwa na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (SAW).


Pogba ambaye anaichezea klabu ya Machester United ya Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza amearifiwa kuchukua hatua hiyo, kufuatia matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu yaliyotolewa na Macron Ijumaa iliyopita.


Inaarifiwa kuwa, Pogba mwenye umri wa miaka 27 na ambaye ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi duniani amechukua hatua hiyo baada ya serikali ya Ufaransa kumpa tuzo ya juu zaidi ya heshima, mwalimu Samuel Paty aliyeuawa hivi karibuni na raia wa Chechnia, kwa kuwaonyesha wanafunzi darasani vibonzo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad (SAW).


Vyombo vya habari vya eneo la Asia Magharibi vimemnukuu  Pogba akisema kitendo hicho ni tusi kwa Waislamu wa Ufaransa, haswa kwa kutilia maanani kuwa, Uislamu ndiyo dini ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi baada ya Ukristo katika nchi hiyo ya Ulaya. 

Hata hivyo baadhi ya vyombo vya habari vya Ufaransa vimekanusha habari hiyo ya kujiuzulu Pogba kuchezea timu ya taifa ya soka ya nchi hiyo.


Kitendo cha Rais Macron kutetea matusi na vitendo vya kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad (SAW) katika jarida la Charlie Hebdo la nchi hiyo kimepelekea nchi mbalimbali za Kiislamu zitoe wito wa kuiadhibu Paris kwa kususia bidhaa za Ufaransa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only