Swala ya Ijumaa kuanza tena Morocco


Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Morocco imetangaza kuruhusia tena swala ya Ijumaa kuswaliwa katika misikiti ya nchi hiyo kuanzia Ijumaa ya wiki hii.

Katika taarifa, wizara hiyo pia imesema idadi ya misikiti ambayo itaruhusiwa kuswaliwa ndani yake sala zote tano imefika 10,000 kote katika ufalme huo wa kaskazini mwa Afrika.


Misikiti Morocco ilifungwa zaidi ya miezi sita iliyopita ili kuzuia kuenea corona.


Taarifa hiyo imesema misikiti ambayo utafunguliwa kwa ajili ya swala tano za kila siku na swala ya Ijumaa imetakiwa kuzingatia kanuni maalumu za kiafya za kuzuia kuenea corona.


Hadi sasa watu 157,000 wameambukizwa corona nchini Morocco huku idadi ya waliofarikia ikiwa ni 2,685.

0 Comments