October 22, 2020

Wanawake Waislamu Uganda wataka waruhusiwe Hijabu katika picha za kitambulisho

Wanawake Waislamu nchini Uganda wamemuandikia barua spika wa bunge la nchi hiyo, Bi Rebecca Kadaga wakitaka mabadiliko katika sharia ili kuwaruhusia wanawake Waislamu wavae Hijabu wakati wanapopigwa picha za vitambulisho.


Ombi hilo limewasilishwa na Namukwaya Aisha mwenyekiti wa jumuiya ya wanawake Waislamu inayojulikana kama Uganda Muslim Women Vision (UMWV). Bi. Aisha amesema wanawake Waislamu Uganda wamekuwa wakikerwa kwa muda mrefu kutokana na kulazimishwa kuvua Hijabu wakati wa kupiga picha za pasipoti, kitambulisha cha taifa na leseni ya kuendesha gari na pia wakati wanapoita katika vituo vya idara ya uhamiaji mipakani au uwanja wa ndege.


Amesema wanawake Waislamu Uganda wamekuwa wakiumia lakini sasa wameamua imetosha na wamevunja kimya chao.


Ameongeza kuwa wanawake Waislamu wanatakuwa kuvaa Hijabu wakati wote wakiwa mbele ya ajinabi kwa mujibu wa mafundisho ya Qurani Tukufu.


Naye Bi Hadija Namyalo ambaye ni mhadhiri wa sharia katika Chuo Kikuu cha Makerere anasema Hijabu ni sehemu ya mavazi ya mwanamko Muilsamu na kumlazimu kuvua vazi hilo ni kumvunjia heshima na kumdhalilisha mbele ya umma. Amesema hataka katika nchi za Magharibi kama vile Marekani na Uingereza wanawake Waislamu wanaruhusiwa kuvaa Hijabu wakati wanapopiga picha za vitambulisho.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only