Msikiti Uholanzi walengwa katika hujuma ya chuki dhidi ya Uislamu

Msikiti katika mji wa Zaandam kaskazini magharibi mwa Indonesia umehujumiwa katika jinai ambayo imetajwa kuwa ya wenye chuki dhidi ya Uislamu.


"Hatujui ni nani hasa aliyetekeleza hujuma hii, lakini tuna wasiwasi. Tuna wasiwasi kuwa, kutokana na kuwa kiza kinaingia mapema wakati wa msimu baridi, wanafunzi wanaofika msikitini kwa ajili ya masomo ya kidini watakumbwa na matatizo," afisa wa msikiti Ismail Genc ameliambia Shirika la Habari la Anadolu.
Genc amesema mlinzi wa msikiti ndiye aliyekuwa wa kwanza kubaini kuwa msikiti umeshambuliwa na kuongezwa kuwa hawajawahi kushuhudia tukio kama hilo.
Amesema hakuna uharibifu mkubwa uliofanyika na kwamba ni madirisha tu yaliyovunjwa katika hujuma hiyo. Amesema uchunguzi kuhusu tukio hilo unaendelea.

Misikiti isiyopungua nchini Uholanzi imekuwa ikikumbwa na mashambulizi tofauti ya chuki dhid ya Uislamu

0 Comments