Shaykh Swaalih Al-Fawzaan: Hukmu Ya Qur-aaniyyuwn Wanaopinga Hadiyth Na Kutosheleka Na Qur-aan Pekee

 Hukmu Ya Qur-aaniyyuwn Wanaopinga Hadiyth Na Kutosheleka Na Qur-aan Pekee

 

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

muislamublog.com

 

 

 

SWALI:

 

Nini hukumu ya wanaojiita  Qur-aaniyyuwn ambao wanazipinga Hadiyth tukufu na wanasema: Tunatosheka na Qur-ani tu?

 

 

JIBU:

 

 

Huko ni kumkufuru Allaah (‘Azza wa Jalla) kwani Hadiyth ni Wahyi wa kutoka kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) nao ni Wahyi wa pili baada ya Qur-aan. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

مَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤

 

Na wala hatamki kwa hawaa. Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

Maneno ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni Wahyi kutoka kwa Allaah ('Azza wa Jalla);    maneno yake yanatoka kwa Rasuli na maana hutoka kwa Allaah ('Azza wa Jalla). Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) 

 

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ

Na lolote analokupeni Rasuli (Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni [Al-Hashr: 7]

 

 

Kisha eti huyu (mtu aliyekusudiwa katika Swali) anasema: “Hakika hakuna isipokuwa sisi tunachukuwa kutoka kwenye Qur-aan tu!”

 

 

 [Fataawaa Shaykh Swaalih Bin-Fawzaan Al-FawzaanAl-Mawqi’ Ar-Rasmiy – Ighaathah Al-Lahfaan 16-06-1439H]            

 

 

0 Comments