Misikiti mitano kuruhusiwa kuswali Ijumaa nchini Singapore

 Misikiti mitano nchini Singapore itaruhusiwa kuwa na waumini 250 kila moja kwa ajili ya swala ya Ijumaa kuanzia wiki hii.


Kwa mujibu wa Baraza la Kiislamu ya Singapore, kufuatia uamuzi huo, idadi ya waumini watakaoruhusiwa kuswali ijumaa nchini humo sasa imeongezeka na kufika 19,365.


Misikiti mingine mitano ambayo imeruhusiwa kuwa na Swala ya Ijumaa ni pamoja na  Al-Islah, Al-Istighfar na Darul Ghufran katika eneo la mashariki, Assyafaah upande wa mashariki, na Al-Khair upande wa magharibi.


Katika kila msikiti kutakuwa na maeneo matano ya ibada na kila ene litakuwa na waumini 50. Mpango huo wa kuruhusu idadi maalumu ya waumini katika misikiti ulizinduliwa mwezi uliopita kwa kuzingatia kanuni za kiafya za kukabiliana na janga la COVID-19 au corona.

0 Comments