Watunisia walaani kufungwa Radio ya Qur’an

Wananchi wa Tunisia wameandamana katika mji mkuu Tunis, kulaani uamuzi wa kuifunga Radio ya Qur’an nchini.


Kwa mujibu wa taarifa, maandamano hayo yamefanyika mbele ya Baraza Kuu la Vyombo vya Habari Tunisia.


Wale walishiriki katika maadanmano hayo wametaka Radio ya Qur’an iruhusiwe tena kuendelea na matangazo yake.


Aidha wametaka Idara ya Mahakama Tunisia iingilie kadhia hiyo.


Hivi karibuni Baraza Kuu la Vyombo vya Habari Tunisia (Conseil Supérieur des Médias) liliiamuru Radio ya Qur’an isitishe matangazo yake kwa madai kuwa haikuwa na leseni.


Mjumbe katika bunge la Tunisia, Saeed al-Jaziri, amelituhumu baraza hilo kuwa limeifunga Radio ya Qur’ani kutokana na ufisadi na ushawishi kutoka nje ya nchi.


Aidha imedokezwa kuwa kuna wanachama wa baraza hilo ambao wanafungaman na utawala wa kiimla uliopinduliwa mwaka 2011. Waandamanaji wanasema uamuzi wa kufunga  Radio ya Qur’ani umetokana na chuki dhidi ya Uislamu.
0 Comments