004-Swahiyh Twibbin-Nabawiy: Aina Za Maradhi

 Swahiyh Twibbin Nabawiy

 

004-Aina Za Maradhi

 

 

 

 بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

 

Kuna aina mbili za maradhi: Maradhi ya nyoyo na maradhi ya miili[1] Na aina mbili hizi zimetajwa ndani ya Qur-aan. Na maradhi ya nyoyo ni aina mbili:

 

a-Maradhi ya shubha na shaka

 

b-Maradhi ya matamanio na upotovu.

 

Na yote hayo yamo katika Qur-aan:

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuhusu maradhi ya shubha:

 

فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ فَزَادَهُمُ اللَّـهُ مَرَضًا ۖ

Ndani ya nyoyo zao mna maradhi na Allaah Akawazidishia maradhi [Al-Baqarah: 10] 

 

Na Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa): 

 

 

   وَلِيَقُولَ الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَالْكَافِرُونَ مَاذَا أَرَادَ اللَّـهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ

Na ili wale waliokuwa na maradhi nyoyoni mwao (ya unafiki, shaka) na makafiri waseme: “Allaah Amekusudia nini kwa mfano huu?”  [Al-Muddaththir: 31]

 

 

Na Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Allaah kuhusu wale walioitwa kuhukumu kwa Qur-aan na Sunnah wakakataa na kupuuza:

 

وَإِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٤٨﴾

Na wanapoitwa kwa Allaah na Rasuli Wake ili Awahukumu baina yao, mara hapo kundi miongoni mwao wanakengeuka.

وَإِن يَكُن لَّهُمُ الْحَقُّ يَأْتُوا إِلَيْهِ مُذْعِنِينَ ﴿٤٩﴾

Na inapokuwa haki ni yao, wanamjia (Rasuli) wakitii.

 

أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ارْتَابُوا أَمْ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ اللَّـهُ عَلَيْهِمْ وَرَسُولُهُ ۚ بَلْ أُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٥٠﴾

Je, mna maradhi katika nyoyo zao, au wametia shaka, au wanakhofu kwamba Allaah na Rasuli Wake watawadhulumu katika kuwahukumu? Bali hao ndio madhalimu. [An-Nuwr: 48-50]

 

 

Haya ni maradhi ya shubha na shaka. Ama maradhi ya matamanio Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anasema:

 

 

يَا نِسَاءَ النَّبِيِّ لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِّنَ النِّسَاءِ ۚ إِنِ اتَّقَيْتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَّعْرُوفًا ﴿٣٢﴾

Enyi wake wa Nabiy!  Nyinyi si kama yeyote yule katika wanawake; mkiwa na taqwa, basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi na semeni kauli inayokubalika. [Al-Ahzaab: 32]

 

Haya ni maradhi ya matamanio ya zinaa. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.

 

 

0 Comments