Imaam Ahmad bin Hanbal - Usiswali Nyuma Ya Anayesema Qur-aan Imeumbwa

  

Mtu alimuuliza Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) akamwambia:

 

"Eee Abaa 'Abdillaah! Je, naweza kuswali nyuma ya mwenye kunywa pombe?
 
Akajibu: "Hapana."

 

Akauliza (yule mtu): "Je, naweza kuswali nyuma ya anayesema Qur-aan imeumbwa?
 
Akajibu (Imaam Ahmad): Subhaana Allaah! Nakukataza kuhusiana na Muislamu na wewe unaniuliza kuhusiana na Kafiri?!

 

[Twabaqaat Al-Hanaabilah, 2/378]

0 Comments