February 5, 2021

Utawala wa Kizayuni wa Israel waendeleza uchimbuaji katika Msikiti wa Al Aqsa

 Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendeleza uchimbuaji chini ya Ukuta wa Nudba na Msikiti wa Al Aqsa ikiwa ni katika njama zake za kuuyahudisha mji wa Quds (Jerusalem).


Fakhri Abu-Dyab mtaalamu wa masuala ya Quds amesema wakuu wa utawala wa Kizayuni wanalenga kujenga jengo jingine katika sehemu ya Ukuta wa Nudba  ili kubadilisha utambulisho wa kihistoria na Kiislamu wa eneo hilo takatifu.

Ameongeza kuwa Wzayuni wanalenga kujenga ukumbi chini ya Ukuta wa Nudba na kisha kujenga njia za chini ya ardhi hadi katika hekalu jipya wanalojenga ili walowezi wa Kizayuni waweze kutekeleza ibada zao katika eneo hilo.

Aidha amesema Wazayuni wanelenga kujenga jengo kubwa ambalo litafika hadi lango la Bab al Maghariba la Msikiti wa Al Aqsa.

Hivi karibuni harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina ilitahadharisha kuhusu mpango wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kubomoa sehemu za Msikiti wa Al Aqsa.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Msikiti wa al-Aqsa ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu umekuwa ukiandamwa na njama mtawalia za utawala vamizi wa Israel, hatua ambazo zinakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only