March 9, 2021

Amnesty yalaani marufuku ‘hatari’ ya nikabu nchini Uswisi

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani kura ya maoni ambayo imeidhinisha marufuku ya vazi la nikabu linalotumiwa na wanawake Waislamu.


Katika taarifa, Amnesty International imesema badala ya kupiga marufuku nikabu, wakuu wa Uswisi wanapaswa kuzingatia hatua ambazo zitawalinda wanawake.


Siku ya Jumapili wapiga kura Uswisi waliunga mkono marufuku ya vazi la nikabu ambapo asilimia 51.2 ya wapiga kura waliunga mkono hatua hiyo na asilimia 48.8 walipinga.


 “Baada ya kura ya kupiga marufu minara ya misikiti, wapiga kura Uswisi kwa mara nyingine wameidhinisha sheria inayobagua jamii moja ya kidini,” amesema Cyriele Huguenot, mkuu wa haki za wanawake katika Amnesty International nchini Uswisi.


Ameongeza kuwa: “Marufuku ya vazi linalofunika uso kikamilifu haiwezi kuwa hatua ya kuwakomboa wanawake. Badala yake ni sera hatari ambayo inakiuka uhuru wa maoni na dini.”


Uswisi imejounga na Ufaransa na Denmark ambazo tayari zimeshapiga marufuku vazi lolote ambalo linafunika uso kikamilifu ambapo sheria hizo zinaonekana kuwalenga Waislamu wanaovaa Hijabu.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only