September 23, 2021

Mamia ya walowezi wa Kizayuni wakivamia Kibla cha Kwanza cha Waislamu

 Vitendo vya chuki na uadui vya walowezi wa Kizayuni vimeendelea baada ya mamia ya walowezi hao wenye chuki na Uislamu kuuvamia Msikiti wa al Aqsa ambao ndicho Kibla cha Kwanza cha Waislamu.Kwa mujibu wa televisheni ya Russia Today, mamia ya walowezi wa Kizayuni jana Jumatano waliuvamia Msikiti wa al Aqsa huku wakipewa ulinzi kamili na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.


Watu walioshuhudia wamesema kuwa, walowezi 539 wamekivamia Kibla cha Kwanza cha Waislamu kwa ulinzi kamili wa jeshi katili la Israel ikiwa ni muendelezo wa siasa za dhulma na uvamizi za utawala wa Kizayuni. Mashuhuda hao wamesema, mamia ya walowezi hao wameuvamia Msikiti wa al Aqsa kwa kutumia mlango wa Bab al Maghariba na kuanza kufanya vitendo vya kuchochea hisia za Waislamu.

Kila wanapovamia maeneo ya Waislamu, walowezi Wazayuni wanapewa ulinzi kamili na askari wa Israel

Uvamizi na mashambulizi ya kila siku yameongezeka sana hivi sasa dhidi ya Msikiti wa al Aqsa. Siku chache zilizopita, Muhammad Hammadah, mwanachama mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS alisema kuwa, harakati hiyo imetoa mwito kwa Wapalestina wote kujiweka tayari kwa ajili ya kukihami na kukilinda Kibla cha Kwanza cha Waislamu.


Mwanamachama huyo mwandamizi wa Hamas aliongeza kuwa, vitendo vya walowezi wa Kizayuni vya kufanya uvamizi wa kinyama dhidi ya Msikiti wa al Aqsa ni kitu ambacho kimepangwa kwa makusudi na utawala wa Kizayuni na kwamba wanajeshi Wazayuni pamoja na polisi wa Israel wamepewa jukumu la kulinda usalama wa kila mlowezi anayevunjia heshima matukufu ya Waislamu na ya Wapalesitna.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only