September 24, 2021

Msikiti mkongwe zaidi India wafunguliwa tenaMsikiti huo ambao ni maarufu kama ‘Cheraman Juma Masjid’ ulijengwa mwaka 629 Miladia (CE) na sasa umerejea katika hali yake ya kawaida kufuatia oparesheni ya kuukarabati ambayo imefanyika kwa muda wa miezi 30 kwa usimamizi wa taasisi ya kiserikali ya  ‘Mradi wa Turathi wa Muziris’.


Inasimuliwa kuwa msikiti huo ulijengwa na Malik Deenar, aliyekuwa ametoka Uajemi (Iran ya leo) kwa amri ya mfalme


Msikiti huo uko katika eneo la Kodungallur Taluk kati mwa jimbo la Kerala. Mbali na kukarabatiwa, pia katika karibu na msikiti huo kumejengwa Jengo la Makumbusho ya Turathi za Kiislamu wa Chera (Kerala ya leo).


Msikiti huo uliharibiwa na Warekani mwaka 1504 Miladia na kisha baada ya hapo kukarabatiwa mara kadhaa.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only