September 25, 2021

RAIS DK.MWINYI ASHIRIKIRI SALA YA KUUSALIA MWILI WA MAREHEMU SULEIMAN NYANGA MSIKITI WA MIEMBENI ZANZIBARRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ya kuhitimisha kisomo cha Hitma ya Marehemu Suleiman Othman Nyanga, ikisomwa na Ustadh.Abdulrahaman Shariff Al-Habshy, baada ya kumaliza kisomo hicha kabla ya kuusalia mwili wa marehemu katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja. na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu.Mohammed Suleiman Nyanga na (kushoto kwa Rais) Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Khalid Ali Mfaume, Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khalid Ali Mfaume.(kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mtoto wa Marehemu Mohammed Suleiman Nyanga na Rais Mstaaf wa Zanzibar Alhaj Dkt. Amani Karume wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa marehemu iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja


WANANCHI na Wauminin wa Kiislam wakiwa wamebeba jeneza likiwa na mwili wa marehemu Suleiman Othman Nyanga baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya kuusalia mwili wa marehemi iliofanyika katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja.


USTADH Abdulrahaman Shariff Al-Babshy akihitimisha kisoma cha hitma ya kumuombea Marehemu Suleiman Nyanga kabla ya kuusalia mwili wa marehemu katika Msikiti wa Miembeni Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only