October 7, 2021

Bin-Aadam Anatokana Na Kizazi Cha Nyani?

Pia ninahitaji kufahamu, tunasoma kuwa Binadamu ametokana na generation ya nyani? je Qur'aan inasemaje ya suala hili.

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu nadharia ya ukuuzi ya Charles Robert Darwin.

Hakika nadharia hiyo haina ithbati yoyote kutoka hata kwa sayansi yenyewe. Bali nadharia hiyo ililetwa na Myahudi Darwin ili kumdhalilisha mwanaadamu. Nadharia hiyo ni potofu na ni kinyume na Qur-aan.

 

Hiyo ni kuwa Allaah Aliyetukuka Anatuambia:

Bila ya shaka Tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa” (at-Twiyn 95: 4). Na Akasema:

Aliyekuumba, Akakuweka sawa, Akakunyoosha” (al-Infitwaar 82: 7). Na Aayah zinazotueleza kuwa mwanaadamu ameumbwa na Allaah Aliyetukuka ni nyingi sana.

Kadhalika hakuna Muislam asiyefahamu kuwa Aadam (‘Alayhis Salaam) ambaye ni mwanaadam wa kwanza, aliumbwa kwa udongo na akatokana naye mkewe Hawwaa na vizazi Haabiyl na Qaabiyl hadi kutufikia sisi leo hii. Sasa huyo nyani katokea wapi hapo?

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only