Jinsi ya kupika Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma, Nyanya Mshumaa Za Kukaanga, Achari

 


Asalaam aleikum ndugu zangu katika iymaan leo katika kipindi chetu cha mapishi tutajifunza jinsi ya kupika Ugali Kwa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma, Nyanya Mshumaa Za Kukaanga na Achari kwanza kabisa andaa vipimo vyako kwa idadi ya walaji 

Vipimo Vya Ugali:

 

Unga wa mahindi - 4 vikombe                               

Maji -  kiasi

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika                                              

 1. Tia maji kiasi katika sufuria wacha yachemke hasa
 2. Tia unga kidogo kidogo huku ukikoroga mpaka ukamatane
 3. Punguza moto huku ukiendelea kuusonga
 4. Endelea kusonga kwa dakika kadhaa mpaka uanze kuchambuka
 5. Kisha mimina kwenye bakuli au sahani na itakuwa tayari  

 

Vipimo Ya Upishi Wa Mchuzi Wa Samaki Wa Kuchoma Wa Nazi

 

 

Samaki:

Samaki wa Nguru - kiasi vipande 5 - 6

Pilipili mbichi - 3

Kitunguu saumu(thomu/galic) - 5 chembe

Tangawizi mbichi - 1 kipande

Bizari ya samaki - 1 kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga - 1 kijiko cha chai

Ndimu - 3 kamua

Chumvi - kiasi

 

 1. Ukipenda mkate samaki vipande kiasi.
 2. Saga vipimo vyote vinginevyo katika mashine. Mchanganyiko ukiwa mzito ongezea ndimu
 3. Changanya pamoja na samaki upake vizuri vipande vya samaki
 4. Acha kwa muda wa nusu saa vikolee mchanganyiko
 5. Panga samaki katika treya ya kupikia ndani ya oveni, kisha mchome (grill) samaki huku ukigeuza hadi viwive.
 6. Epua weka kando.

 

Mchuzi:

Nyanya/tungule - 3

Kitunguu - 2

Bizari ya manjano/haldi - ¼ kijiko cha chai

Mafuta - 3 vijiko vya supu

Tui la nazi zito - 3 vikombe

Chumvi - kiasi

 

 1. Katakata vitunguu na nyanya vidogodogo (chopped) weka kando
 2. Weka mafuta katika karai au sufuria, kaanga vitunguu hadi vianze kugeuka rangi
 3. Tia nyanya kaanga pamoja na tia bizari ya njano/haldi .
 4. Tia tui la nazi, chumvi koroga .
 5. Mwishowe tia vipande vya samaki na rojo lake litakalobakia katika treya, mchuzi uko tayari.

0 Comments