October 2, 2021

Maelfu ya Wapalestina wasali Sala ya Ijumaa Quds licha hatua kali za Israel za kuwazuia

 Idara ya Waqfu ya Quds imetangaza kuwa, licha ya njama, mibinyo, ukandamizaji na hatua kali za jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel, lakini Wapalestina wasiopungua 50,000 jana walitekeleza ibada ya kisiasa na kimaanawi ya Sala ya Ijumaa katika msikiti wa al-Aqswa na hivyo kwa mara nyingine tena kusambaratisha njama za Wazayuni maghasibu.Pamoja na hayo, mamia ya Wapalestina hawakuweza kusali Sala ya Ijumaa katika msikiti huo baada ya jeshi la utawala dhalimu wa Israel kuweka vizuizi na ulinzi mkali katika baadhi ya maeneo na kuwazuia Wapalestina kupita kwa ajili ya kwenda katika msikiti wa al-Aqswa.


Aidha baada ya Sala ya Ijumaa, maelfu ya Wapalestina waliandamana na kulaani jinai na sera za utawala wa Kizayuni wa Israel hususan kuendelea ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahuudi katika maeneo ya Wapalestina.

Jeshi la Israel likiwa na lengo la kukabiliana na waandamanaji hao lilituma ndege isiyo na rubani ambayo ilikuwa ikirusha mabomu ya gesi ya kutoa machozi. Waandamanaji hao walifanikiwa kuinasa ndege baada ya kudondoka na kuipondaponda.


Katika miaka ya hivi karibuni walimwengu wameshuhudia kuongezeka njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Palestina hususan ujenzi wa vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni ambao lengo lake ni kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Palestina.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only