Mawlid: Vizuizi 12 Dhidi Ya Kusherehekea Kuzaliwa Kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 Shukrani ni za Allaah, na rahma zimuendee Rasuli wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambaye ni mbora wa viumbe wote …

 

Ninataka kuweka (wazi) mbele ya msomaji, vizuizi (nukta) vifuatavyo kuhusiana na washerehekeaji wa siku ya kuzaliwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aailihi wa sallam), ikitajwa tendo lao la kufanya hivyo, kwa mujibu wa Shari’ah ya Kiislamu; kitendo cha haki iliyoruhusiwa (Halali) au dhidi ya Shari’ah (Haramu). Kwa maneno mengine, je inastahiki kupatiwa adhabu? Zaidi ninamuomba Allaah, kwamba makala hii kuwa ni yenye manufaa kwa wote.

 

Kizuizi Cha Kwanza

Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Amemtaka Nabiy  (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata yale ambayo Allaah Amemshushia na sio kubuni maelekezo ya ‘uongo’, Anasema katika maneno Yake ndani ya Qur-aan:

 ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِّنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ

Kisha Tukakuwekea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) shariy’ah ya mambo, basi ifuate, na wala usifuate hawaa za wale wasiojua. [Al-Jaathiyah: 18].

 

Matendo ya ibada ya Kiislamu hayabadiliki, hayaathiriki na yenye kudumu kama vile yalivyoshushuwa kwa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Akili haiwezi kutumika kuingilia ibada hizo. Hivyo, Allaah Amemuelekeza Nabiy wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kufuata wahyi (tu) katika nafasi nyingi. Kwa mfano maneno haya ya Allaah:

وَإِذَا لَمْ تَأْتِهِم بِآيَةٍ قَالُوا لَوْلَا اجْتَبَيْتَهَا ۚ قُلْ إِنَّمَا أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰ إِلَيَّ مِن رَّبِّي ۚ هَـٰذَا بَصَائِرُ مِن رَّبِّكُمْ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ

Na usipowaletea Aayah (muujiza, ishara) husema: Kwanini hukuibuni? Sema: Hakika hapana ila nafuata yale nilofunuliwa Wahy kutoka kwa Rabb wangu. Hii (Qur-aan) ni nuru za elimu na umaizi kutoka kwa Rabb wenu, na ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini. [Al-A’raaf: 203].

 

Zaidi, Wanachuoni sahihi wa Uislamu wameamua kwamba: ibada ni kwa mujibu tu wa kufuata Qur-aan na Sunnah, na sio kuzua.

 

 

Kizuizi Cha Pili

Hakika Allaah Amewashushia ihsani kubwa Waumini kwa kuwaletea Nabiy wake Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na sio sherehe ya siku yake ya kuzaliwa hata kidogo. Kwamba yale ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) amesema ndani ya Kitabu Chake “Qur-aan” (ndio ya kufuatwa). Aayah zinazozungumzia kiini hichi itakuwa ni:

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao, Rasuli miongoni mwao, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah); japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana. [Al-‘Imraan: 164].

 

 

Kizuizi Cha Tatu

Kizazi cha mwanzo cha Waumini ambacho kilikuwa ni cha Swahaba wa Nabiy (ambao tumehimizwa kuwafuata na kuchukua ufahamu wao wa kipi kilichotolewa maana ndani ya Aayah za Qur-aan na Hadiyth kuwa ndio kigezo cha ufahamu wetu wa Uislamu) hawakupatapo kuongeza kitu chochote katika ibada zao za kawaida katika siku ya kuzaliwa kwa Nabiy. Iwapo wameongeza cha ziada, hakuna shaka yoyote kwamba kingetufikia sisi. Kwa sababu walikuwa ni wenye hamu na hima ya kuwa na elimu sahihi kab

0 Comments