Misikiti minne wachomwa moto nchini india

Wahindu wenya misimamo mikali katika jimbo la Tripura kaskazini mashariki mwa India wamewahujumu Waislamu na kuharibu misikiti minne kwa sababu ya kulipiza kisasi kutokana na kile wanachodai ni kusumbuliwa Wahindu katika nchi jirani ya Bangladesh.


Kufuatia hali hiyo, wakuu wa eneo hilo wamepiga marufuku mijimuiko ya watu zaidi ya wanne na kuonya kuhusu jumbe chochezi katika mitandao ya kijamii.

Jimbo la Tripura lina mpaka wa kilimota 850 na nchi ya Bangladesh ambayo wakazi wake wengi ni Waislamu. Hivi karibuni nchini Bangladesh watu waliokuwa na hasira walivamia hekalu la Wahindu ambapo watu saba walipoteza maisha katika ghasia hizo.

Machafuko hayo yaliibuka baada ya kuenea klipu iliyooneysha Msahafu ukiwe umewekwa katika goti la kijimungu cha Kihindu jambo ambalo liliwakasirisha Waislamu na kuibua ghasia katika wilaya 12 nchini Bangladesh.

Jimbo la Tripura nchini India linatawaliwa na chama cha waziri mkuu wa India cha Bharatiya Janata (BJP) ambacho kinalaumiwa kuwa na misimamo mikali ya Kihindu.

Waislamu nchini India wanakabiliwa na hujuma za mara kwa mara kutoka kwa Wahindi wenye misimamo mikali tokea mwaka 2014 tokea chama cha BJP kiingie madarakani.

0 Comments