October 7, 2021

Msweden aliyemvunjia heshima Mtume Muhammad SAW aangamia katika ajali mbaya barabarani

 Vilks (75) aliaga dunia jana Jumapili, baada ya gari lililokuwa limembeba akiwa pamoja na maafisa wawili wa polisi kugongana ana kwa ana na lori katika mji wa Markaryd, kaunti ya Kronoberg kusini mwa Sweden.Carina Persson, mkuu wa polisi wa kaunti hiyo amethibitisha habari hiyo na kueleza kuwa, Vilks pamoja na askari polisi wawili waliokuwa wakimlinda wameangamia katika ajali hiyo ya jana.


Ameongeza kuwa, magari mawili yaliyohusika katika ajali hiyo ya jana yameteketea moto, lakini dereva wa lori amenusurika kifo, ingawaje amejeruhiwa vibaya.


Vilks ambaye alichora vibonzo vilivyomjunjia heshima Mtume SAW na kupelekea kuibuka maandamano kote duniani mwaka 2007, ameponea chupu chupu kuuawa mara kadhaa.


Moja ya katuni za kukirihisha alizochora raia huyo wa Denmark na kuwaghadhabisha mno Waislamu kote duniani, ni ile ya eti kichwa cha Mtume Mtukufu, kilichoungwa na mwili wa mbwa.


Nchi za Magharibi kwa miaka mingi sasa zimekuwa zikiunga mkono na hata kuyashajiisha majarida ya bara Ulaya kuchora vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Mtukufu wa Uislamu, Muhammad SAW.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only