October 7, 2021

Ongezeko la hujuma dhidi ya Waislamu wa Assam, India

 

Kwa mujibu wa taarifa Wahindi hao wanawashambulia Waislamu kwa madai kuwa ni wahajiri walioingia India kinyume cha sheria kutoka nchi jirani ya Bangladesh. Lakini imebainika kuwa Waislamu hao wanalengwa pamoja na kuwa ni raia rasmi wa India hivyo kinachoendelea ni chuki za kidini.


Klipu kadhaa za video zimeenea na kuoneysha Waislamu wanavyokandamizwa na kunyanyaswa karibu kila siku.


Hivi karibuni pia wanajeshi wa India waliharibu mamia ya nyumba katika kijiji kimoja eneo hilo ambapo kwa uchache mototo aliuawa na maelfu ya watu kuachwa bila makazi.


Kwa muda mrefu sasa chama tawala India cha BJP, chenye misimamo mikali ya Kihindu, kimekuwa kikitekeleza kampeni ya makusudi dhidi ya Waislamu wa eneo la Assam ambao ni zaidi ya asilimia 33 ya wakazi wa jimbo hilo la kaskazini mashariki.


Mwaka 2018, serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi iliwapokonya uraia mamilioni ya Waislamu wa Assam kwa madai kuwa ni wahajiri haramu kutoka nchi jirani ya Bangladesh.


Kuanzia Septemba 20 oparesheni ya kuwatimua Waislamu kutoka nyumba zao imeanza na hadi sasa familia 800 zimelazimishwa kuondoka.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only