October 7, 2021

Qatar yaondoa kanuni ya kutokaribiana Misikitini

 

Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar imefuta kanuni ya kutokaribiana na kutogusana (social distancing) misikitini wakati wa Sala sambamba na kufungua tena maeneo ya kutawadha.

Katika taarifa, wizara hiyo imetangaza kuwa kuanzia Jumapili wiki hii, vizuizi vitokanavyo na COVID-19 vimepungua katika misikiti ya nchi hiyo na hivyo sasa hakutakuwa tena na kanuni ya kutokaribiana misikitini. Halikadhalika maeneo ya kutawadha misikitini sasa yatakuwa wazi kutumiwa na Waislamu wanaofika misikitini.


Aidha Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu nchini Qatar imesema afya ya watu wanaofika misikitini itachunguzwa kupitia aplikesheni maamulu ya simu za mkononi ambayo aitaweza kubainisha wale waliopata chanjo jamili ya COVID-19. Vile vile ni sharti sasa kwa kila anayeingia msikitini kubeba mkeka binafsi wa kusali sambamba na kutumia barakoa wakati wote akiwa msikitini.


Hatua hizo za kupungu vizuizi misikitini zimechukuliwa baada idadi ya maambukizi ya COVID-19 kupungua kwa kiasi ikikubwa nchini Qatar.

Post a Comment

Whatsapp Button works on Mobile Device only