Al Azhar yaanza tena vikao vya Qur'ani vya kuhuduria ana kwa ana

 Msikiti wa Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar umeanza tena darsa za Qur'ani za kuhudhuria ana kwa ana baada ya marufuku yam waka moja na nusu kutokana na janga la COVID-19.


Darsa za kuhifadhi Qur'ani zimenza Jumanne katika kategoria tatu na pia kuna darsa maalumu za watoto ambapo wanafunzi wamhudhuria ana kwa ana na waalimu wao.


Dkt. Abdel Moneim Fuad, msimamisi wa shughuli za kielimu katika Kituo cha Kiislamu cha Al Azhar amesema vikao vya kuhifadhi Qurani vitafanyika kama ilivyopangwa.


Aidha amesema watalenga kuwavutia wanafunzi sasa baada ya vizuizi vya COVID-19 kuondolewa.


Hivi karibuni  Wizara ya Wakfu nchini Misri imetangaza kuwa darsa za kuhifadhi Qur'ani ndani ya misikiti kwa kuhudhuria ana kwa ana waalimu na wanafunzi zitaanza tena kote katika nchi hiyo.


Wazri wa Wakfu Sheikh Mohamad Mokhtar Gomaa amesema  suhula za kisasa zitatumika darasani kuhu wanaoshiriki wakitakiwa kuzingatia sheria za kiafya za kuzuia kuenea COVID-19. Amesema misikiti yote itatenga maeneo maalumu ya kufundisha Qur'anikwa watoto kwa sharti kuwa suhula zinazohitajika zinanunuliwa.

0 Comments