Jimbo la Selangor Malaysia laafiki kuongeza idadi ya wanaosali Ijumaa misikitini


Sultan Sharafuddin Idris Shah amesema baada ya kupungua maambukizi ya COVID-19 kuna haja ya kuruhusu idadi kubwa ya waumini kushiriki katika Sala ya Ijumaa. Amesema: "Kwa mfano Msikiti wa Sultan Salahuddin Abdul Aziz Shah sasa utakuwa na idhini ya kuwaruhusu waumini 3,500 badala ya 2,000 hivi sasa."

Katika ujumbe kupitia ukurasa wa Facebook wa Ofisi ya Kifalme ya Selangro, Sultan Sharafuddin Idris Shah amesema misikiti ya wilaya itaruhusiwa kuongeza idadi ya wanaoswali kwa kuzingatia ukubwa wa kila msikiti. Amesema data za wanaopoteza maisha kutokana na COVID-19 zinaonyesha idadi hiyo sasa ni chini ya 10 kwa siku.

Hatahivyo amewakumbusha waumini kuwa wanapaswa kuendelea kuzingatia kanuni za kiafya za kukabiliana na COVID-19 ambazo zimewekwa na Wizara ya Afya na Idara ya Kiislamu ya Selangor wakati wote wakiwa wanatekeelza ibada misikitini.

0 Comments