Misikiti Misri yapewa siku 10 kuondoa masanduku ya misaada

Wizara ya Wakfu ya Misri imetangaza Ijumaa kuwa masanduku ya misaada ni marufuku katika misikiti kote Misri.


"Ni marufuku kukusanya pesa au kupokea pesa taslimu katika misikiti kwa sababu yote ile. Aidha ni marufuku kabisa kuwa na masanduku ya kupokea misaada ndani nan je ya misikiti," imesema amri ya Wizara ya Wakfu ya Misri.


Waziri wa Wakfu Misri Sheikh Muhammad Mukhtar Gomaa ameipa misikiti yote nchini humo muda wa siku 10 kuondoa masanduku ya kupokea misaada ya fedha taslimu. Amesema sababu ya kutolewa masanduku hayo ya kupokea fedha taslimi ni kuhakikisha kuwa kuna uwazi wa kiwango cha juu katika masuala ya fedha. Mkuu wa Idara ya Masuala ya Kidini katika Wizara ya Wakfu Misri Hisham Abdul Azizi amesema uamuzi huo haumaanishi kutoa misaada misikitini ni marufuku bali lengo la uamuzi huo ni kuweka utaratibua wa kisheria katika ukusanyaj misaada. Ameongeza kuwa uamuzi huo umekuja ili kuwezesha misaada kupokewa kwa njia za kidijitali.


Misikiti na maeneo ya ibada kote Misri inakadiriwa kuwa 140,000 na waumini wanaofanya ibada kawaida huweka misaada yao katika masanduku. Hivi sasa Wiara ya Wakfu Misri inatazamiwa kutangaza utaratibu wa kutoa misaada kwa njia za kidijitali misikitini.

0 Comments