Ufaransa yapinga kampeni ya uhuru wa kuvaa Hijabu Ulaya

Serikali ya Ufaransa inapinga kampeni ya uhuru wa kuvaa Hijabu katika nchi za Umoja wa Ulaya jambo ambalo limepelekea video na picha za kampeni hiyo kufutwa katika mtandao wa Twitter.


Taarifa zinasema serikali ya Ufaransa inazuia kampeni inayosimamiwa na Baraza la Ulaya, ambalo ni kitengo cha Umoja wa Ulaya,  inayolenga kuhimiza wanawake wawe na uhuru wa kuvaa vazi la staha la Hijabu.


Katibu wa Masuala ya Vijana Ufaransa Sarah El Hairy amenukuliwa akisema kuwa ameshtushwa na kampeni hiyo na mabango yanayotumiwa katka mtandao wa kijamii wa Twitter. Akizungumza Jumanne, amesema kampeni hiyo ni "kinyume cha thamani za Kifaransa na hivyo Ufaransa inaipinga na ndio sababu inasitishwa leo."


Amedai kuwa Ufaransa inaunga mkono uhuru wa dini na kuabudu lakini inapinga kampeni ya kuunga mkono Hijab. Kampeni hiyo sasa imefutwa kutokana na ushawishi wa Ufaransa katika Umoja wa Ulaya.


Mabango yaliyokuwa yanaonyesha wasichana wakiwa wamevaa mitandio ya Kiislamu yameondolewa katika kursa za Twitter mara baada ya kampeni hiyo kuzindiliwa.


Mnamo Oktoba 28, Baraza la Ulaya lilizindua kampeni ya uhuru wa kuvaa hijabuambapo kulikuwa na nara na kaulimbiu kama vile, 'umaridadi uko utofauti, kama ambavyo uhuru uko katika Hijabu'. Kampeni hiyo ilikuwa inaleng akukabiliana na wimbi la chuki dhidi ya Uislamu kwa kuelimisha jamii kuhusu Hijabu.


Katika miaka ya karibuni wimbi la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa limeshadidi ambapo hasa katika uongozi wa Emmanuel Macron ambapo Waislamu wengi wamekuwa waiandamwa kwa mashinikizo na vitendo vya bughuda na mauadhi na hata wakati mwingine matukufu ya dini yao kutusiwa na kuvunjiwa heshima.


Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

0 Comments