Wenye chuki dhidi ya Uislamu wahujumu misikiti mitatu Ufaransa

 Misikiti mitatu Ufaransa imehujumiwa na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu Jumapili katika miji ya Montlebon, Pontarlier, na Roubaix.


Waliotekeleza jinai hizo walichora misalaba na maandishi yaliyo dhidi ya Uislamu katika kuta za misikiti hiyo inayosimamiwa na Idara ya Uturuki ya Jumuiya ya Kiislamu na Masuala ya Kidini (DITIB) nchini Ufaransa.


"Tunalaani hujuma dhidi ya misikiti yetu," imesema taarifa ya DITIBA. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, jitihada zimeanzishwa za kukarabati maeneo yaliyo haribiwa katika misikiti hiyo.


Aidha taarifa hiyo imesema: "Tunawashukuru maafisa wa Ufaransa kwa ushirikiano na pia tunatoa shukrani kwa watu wa Ufaransa ambao wametuunga mkono. "


Vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu  vimeongezeka nchini Ufaransa na kote Ulaya katika miaka ya hivi karibuni. Wazungu wa mrengo wa kulia wenye misimamo mikali dhidi ya raia wa kigeni ndio wanaochochea zaidi hisia za chuki dhidi ya Uislamu au Islampohobia katika nchi za Ulaya. Katika kutetea jinai zao hizo, wanatumia visingizo vya hujuma za kigaidi za makundi ya ISIS na Al Qaeda pamoja na ongezeko la wakimbizi.


Katika miaka ya karibuni wimbi la chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa limeshadidi ambapo hasa katika uongozi wa Emmanuel Macron ambapo Waislamu wengi wamekuwa waiandamwa kwa mashinikizo na vitendo vya bughuda na mauadhi na hata wakati mwingine matukufu ya dini yao kutusiwa na kuvunjiwa heshima.


Ufaransa ina idadi kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya. Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2016, kuna zaidi ya Waislamu milioni 5.7 Ufaransa ambao ni takribani asilimia 8.8 ya watu wote nchini humo.

0 Comments