China Baba amkata mwanae vidole baada ya Kusilimu


Hadithi ya kijana ambaye ni Mchina kusilimu na kuwa Muislamu ilisimuliwa katika Msikiti wa Chuma wa China. Hadithi hiyo ilitumwa na Abdul Wahab Saleem kwenye Facebook yake.


Muislamu unayeweza kumuona leo wakati mmoja alikuwa Mbuddha ambaye alitoka katika familia ya Kibuddha inayozingatiwa sana na kuwa na msimamo mkali kuhusu dini yao hiyo. Kukabiliana na changamoto za imani yake mpya na familia yake ilikuwa changamoto yake kubwa baada ya kusilimu.


Baada ya kujua kwamba mtoto wake amesilimu, baba yake wa Kibudha alimgeuka.


Baba yake alimkata vidole vyake ili kumlazimisha kuacha Uislamu. Mja huyo kijana alibaki imara katika imani yake.

0 Comments