Muigizaji kutoka India Sanam Chaudhry Achana na Uigizaji, Amrudia ALLAAH.

Muigizaji Sanam Chaudhry ambaye anafahamika kwa uhusika wake kama Anjum katika tamthilia ya Ghar Titli Ka Par alitangaza kwamba kwa sasa anapiga hatua kuelekea karibu na safari yake ya kiroho na kurejea kwa mola wake.


Sanam Chaudhry alishiriki habari muhimu kwenye akaunti yake ya Instagram siku moja tu kabla ya siku yake ya kuzaliwa ya 30. Katika video aliyoshiriki katika mtandao wa imstagram, familia yake imeonekana ikituma maua na keki kama njia ya kuunga mkono uamuzi wa mwigizaji huyo.


Kukamilisha video hiyo, mwigizaji huyo aliandika shukrani zake kwa msaada wa familia yake ambayo aliiita "ya kutia moyo".


Mke wa msanii wa muziki wa Pakistani Somee Chohan pia amewahi kushiriki aya kutoka Surah Al-Azab, ambayo inawashauri wanawake wa Kiislamu kujistiri. Aliandika katika maelezo “Nilipata majibu yangu kutokana na kujifunza Qur-ani…Na ninarejea kwa moyo wangu wote Allah tera Shuker (asante).Ingawa hajatangaza rasmi kuacha showbiz, mwigizaji huyo wa Mere Meherban amefikia hatua ya kufuta picha kadhaa kwenye Instagram yake na kuacha picha chache tu za sherehe ya harusi yake.

Si hivyo tu, lakini mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 30 pia amebadilisha wasifu wake wa Instagram kwa maneno haya: "Muislamu, mama, na mwanafunzi wa Uislamu, Dini ya Muumba wetu Allaah".


Hatua ya Chaudhry hapo awali ilifanywa na mwigizaji wa zamani wa India na mwanamitindo Sana Khan. Sana, ambaye anafahamika kwa uchezaji wake wa dansi katika filamu na kipindi cha TV cha Bigg Boss, alitangaza uamuzi wake wa kuacha ulimwengu wa burudani wa Bollywood ili kuongeza maarifa yake ya kidini na kuendelea na safari yake kuelekea katika Uislamu mwaka jana.

0 Comments