Saudi Yapiga marufuku kundi la Tablighi Jamat

 Saudi Arabia yapiga marufuku Tablighi Jamat katika Ufalme wake


Saudi Arabia imepiga marufuku Tablighi Jamat nchini humo ikiiita kuwa ni "hatari kwa jamii" na ni "moja ya milango ya ugaidi".


Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Saudia Dk. Abdullatif Alsheikh aliiagiza misikiti iliyoswali swala ya Ijumaa kutenga khutba ya Ijumaa ijayo ili kuwaonya dhidi ya kundi la Tablighi Jamat na Da’wah.


Kwa nini Tablighi Jamat imepigwa marufuku Saudi Arabia?

waziri huyo Aliwataka Maimamu wajumuishe mada zifuatazo katika khutba ya Ijumaa kuhusu Jamat ya Tablighi;


1- Kutangaza upotofu,  na hatari ya kundi hili, na kwamba ni moja ya milango ya ugaidi, hata kama wanadai kinyume chake.

2- wataje makosa yao makubwa.


3- yatajwe hatari yao kwa jamii.


4- Taarifa kwamba ushirikiano na makundi ya washiriki, ikiwa ni pamoja na Tablighi na makundi ya Da'wah ni marufuku nchini Saudi Arabia.

Tablighi Jamat ni nini?

Tablighi Jamaat ni kundi la kujitolea la Kiislamu ambalo linalenga katika kuwahimiza Waislamu kufuata mfumo safi wa Uislamu.


Tablighi = Mhubiri.

Jamat = Kundi.

Wanadai kutumia makundi mbalimbali ya watu (waitwao Jamat) duniani kote kwenye misikiti mbalimbali ili kuwahubiria wengine kuhusu Uislamu.


0 Comments