Taasisi ya The Islamic Foundation yatembelewa na One Ummah Charity


Taasisi ya oneummahcharity  kutoka nchini Uingereza imefanya ziara makao makuu ya Taasisi ya The Islamic Foundation mjini Morogoro na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Taasisi ya The Islamic Foundation Aref Nahdi akatumia nafasi hiyo kuuelezea uongozi wa One Ummah shughuli nyinginezo mbalimbali zinazofanywa na Taasisi ya The Islamic Foundation.

Kwa upande wake mkuu wa mipango wa Taasisi ya One Ummah Naveed Ahmed akatoa salamu za taasisi hiyo sambamba na kupongeza shughuli zinazofanywa na Taasisi ya The Islamic Foundation kuisaidia jamii ya kitanzania katika nyanja mbalimbali na kuanza mikakati ya kufanya kazia pamoja na taasisi hii.

Ziara ya Taasisi ya @oneummahcharity  kwa The Islamic Fondation ni muendelezo wa ziara mbalimbali za taasisi kutoka nje ya nchi kuitembela Taasisi hii kwakuwa ni moja kati ya Taasisi zinazosifika ndani na nje ya nchini kutokana na utendaji kazi wake wa kuisaidia jamii.

0 Comments