Wanawake Waislamu waruhusiwa kuvaa Hijabu katika mahakama za Ubelgiji

 Ubelgiji imeondoa marufuku ya uvaaji vazi la stara ya mwanamke wa Kiislamu Hijabu iliyokuwa imewekwa kwa wale wanaoingia katika mahakama za nchi hiyo.


Ikiitikia onyo la Baraza la Mawaziri la Ulaya, Ubelgiji imefanya marekebisho ya kifungu cha 759 cha kanuni ya adhabu ya nchi hiyo, inayokataza uvaaji wa vazi la heshima la hijabu mahakamani.


Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke ambaye ni Mwislamu kuomba kufanya kazi Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu mwaka 2018 na kulazimishwa kuvua hijabu yake, lakini alikataa kufanya hivyo kwani ni kinyume na itikadi na mafundisho ya dini yake ya Kiislamu.


Mahakama ya Strasbourg imeamua kuwa, uamuzi wa Ubelgiji kumzuia mwanamke Mwislamu kuvaa Hijabu mahakamani ni "kukiuka uhuru wa dini na wa kuabudu". Majaji pia waliamua kwamba Hijabu inaweza kuvaliwa kwa msingi wa "uhuru wa imani".


Baadhi ya majaji wamesema kwamba marufuku hiyo inapaswa kutekelezwa. Sheria hiyo ilitungwa kipindi ambacho kila mtu nchini Ubelgiji alivaa kofia, ambayo ilimtaka mtu yeyote anayefanya kazi mahakamani kuwa huru, kuwa kimya na kuonesha heshima." Kelstman, mkurugenzi wa Kituo cha fursa sawa, alisema: "Mabadiliko yamefanyika hatimaye. Tunakaribisha hatua hii kuelekea haki za binadamu."


Serikali na mahakama za nchi mbali mbali za Ulaya zimekuwa zikipitisha sheria kali dhidi ya raia Waislamu wa nchi hizo ambapo Ubelgiji na Ufaransa ni miongoni mwa mataifa ya bara hilo ambayo mara kwa mara yamekuwa yakkipasisha sheria zilizo dhidi ya waislamu kama kkuvaa vazi la stara ya wanawake wa Kiislamu hijabu.

0 Comments