MAPISHI : Jinsi ya kupika Pizza Ya Mboga

 

Vipimo 

Unga - 4 Vikombe

Maziwa ya unga - 2 vijiko vya supu

Mafuta ya zaituni - ½ kikombe

Hamira - 1 kijiko cha supu

Chumvi - kiasi

Sukari - 1 kijiko cha chai

Maji dafu dafu - 2 kikombe

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga.
  2. Ufunike na uache uumuke.

Sosi ya Pizza

Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo - 1

Kitunguu saumu(thomu) iliyokatwa ndogo ndogo - 3 chembe                      

Sosi ya HP - 3 vijiko vya supu

Sosi ya tomato - 3 vijiko vya supu

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Oregano - ½ kijiko cha chai

Parsley (ukipenda) - ½ ukipenda

Namna ya kutengeneza Sosi

  1. Kaanga vitunguu kisha tia thomu, na vitu vyote iwe sosi.
  2. Epua kwenye moto.

Vitu vya kujaza juu ya pizza

 

Nyanya zilizokatwa vipande vipande

Pilipili mboga iliyokatwa ndogo ndogo

Chembe za mahindi kiasi

Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi

Cheese ya Mazorella

 

Namna ya kutayarisha na kupika

  1. Fanya madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu size kama kwenye picha.
  2. Paka sosi juu ya unga
  3. Tia kiteo upendacho
  4. Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza
  5. Mwagia cheese
  6. Pika katika oveni kwa muda dakika 20 moto wa 350 C au zaidi hadi ziwive pizza.

Kidokezo:

 

Upendavyo katika hivi au vyovyote vinginevyo kujaza juu ya pizza

Tuna  

Nyama ya kusaga iliyopikwa  

Kuku aliyekaushwa na kukatwa vipande vipande  

Sauage zilizokatwa  

Salami  

Vipande vya nanasi

 

0 Comments