Waziri mkuu nae amtembelea Muft wa Tanzania Kumpa pole

 


Na : Abdul Latif Makbel 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 5, 2022 amemjulia hali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Bin Zubeir ambaye amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) mkoani Dar es salaam kwa matibabu.

Akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI  Dkt. Samweli Swai, Mheshimiwa Majaliwa amemtakia pona ya haraka Mufti wa Tanzania Abubakar Bin Zubeir ili arejee katika majukumu yake ya kazi.

Naye, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Bin Zubeir amewashukuru madaktari na wahudumu kwa huduma aliyoipata akiwa hospitalini hapo.

0 Comments