03-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Akitoharika Nifaas Kabla Ya Siku Arubaini Je Aswali Na Afunge?

 

Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 

03-Akitoharika Nifaas Kabla Ya Siku Arubaini Je Aswali Na Afunge?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Muislamublog.com

 

 

SWALI:

 

 

Je yapasa kwa mwanamke mwenye nifaas afunge na kuswali akitoharika kabla ya arubaini?

 

 

JIBU:

 

 

Naam. Pindi akitoharika mwenye nifaas kabla ya  arubaini basi inawajibika kwake Swawm ikiwa katika Ramadhwaan na itampasa kuswali pia na inajuzu kwa mumewe kujamii naye kwani ametoharika hana kizuizi cha Swawm wala kinachomzuia Swalaah na kupasa kwake kufanya jimai.

 

0 Comments