04-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Hedhi Yenye Kawaida Ya Siku Sita Au Saba Kisha Ikaendelea Siku Chache

 Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas

 


04-Hedhi Yenye Kawaida Ya Siku Sita Au Saba Kisha Ikaendelea Siku Chache

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Muislamublog.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Ikiwa ada ya mwezi ya mwanamke ni siku nane au saba katika mwezi kisha ikaendelea mara moja au mara mbili au zaidi ya hapo hukumu ni ipi?

 

 

JIBU:

 

Ikiwa ada yake mwanamke huyu ni siku sita au saba kisha ikaongezeka muda na ikawa ni nane au tisa au kumi au kumi na moja basi atabaki kutoswali hadi atoharike  na hiyo ni kwa sababu Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  hakuweka mpaka maalum katika hedhi na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  Anasema:

 

 وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى   

Na wanakuuliza kuhusu hedhi. Sema: “Hiyo ni dhara;  [al-Baqarah: 222]

 

 

Madamu damu hii itaendelea kubaki, basi mwanamke ataendelea kubaki katika hali yake hadi atoharike kisha ataoga josho (ghuslu) na kuswali. Na akija katika mwezi mwengine akiwa imepunguka kuliko hivyo basii ataoga josho  atakapotoharika hata kama sio katika muda ule uliopita. La muhimu ni kuwa madamu atakuwa bado ni mwenye hedhi hatosali ikiwa hedhi hiyo inawafikiana na muda uliotangulia au imeongezeka au kupungua basi akitoharika tu anawajibika kuswali.

0 Comments