05-Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Damu Ya Nifaas Lazima Ifikie Siku Arubaini Au Ikikatika Ametoharika?

 Fataawaa Mas-ala 60 Kuhusu Hedhi Na Nifaas


 

05-Damu Ya Nifaas Lazima Ifikie Siku Arubaini Au Ikikatika Ametoharika?

 

Imaam Ibn 'Uthaymiyn (Rahimahu-Allaah)

 

Muislamublog.com

 

 

SWALI:

 

Mwanamke mwenye Nifasi atasubiri siku arubaini haswali wala hafungi au mazingatio ni kukatika kwa damu. Muda wa kuwa damu imekatika anaweza kujitoharisha na kuswali?

 

Na muda upi ni uchache wa kutoharika?

 

 

JIBU:

 

Mwenye Nifasi hana muda maalum lakini muda wa kuwa damu bado ipo atasubiri, hatoswali na hatofunga na hatoingiliana na mume wake. Na akiona ametoharika hata kabla ya arubaini hata kama hakukaa siku tano au kumi basi ataswali na kufunga  na kuingiliana na mumewe wala hakuna ubaya hivyo.

  

La muhimu ni kwamba Nifaas ni jambo lenye kuhisiwa  inahusiana  hukumu yake kwa kuwepo kwake au kutokuwepo. Madamu (damu) ipo basi hukumu yake itathibitika,  na muda wa kuwa ametoharika ataachana na hukumu yake.

 

 

Hata hivyo ikizidi zaidi ya siku sitini basi mtu mwenyewe atakuwa ni 'Mustahaadhwah' atakaa na kufuata ada ya hedhi yake tu kisha atakoga na kuswali.

0 Comments