Bomu la Mikono Limelipuka Katika Msikiti Mkubwa Zaidi wa Kabul na kujeruhi watu 6

Bomu la kurushwa kwa mkono lililipuka katika msikiti maarufu zaidi wa Kabul wakati waumini walipokuwa wakifanya ibaadah yao ya alasiri siku ya Jumatano. Vyombo vya habari kadhaa vya kigeni viliripoti kwamba waumini wasiopungua sita walijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo lisilo la kuwajibika.


Kwa mujibu wa msemaji wa polisi wa Kabul Khalid Zadran, mtu mmoja anayeshukiwa kuhusika na shambulio la bomu la kutupa kwa mkono kwenye Msikiti wa Pul-e-Khisti amekamatwa katika eneo la tukio.


Bado hakuna aliyedai kuhusika na tukio hilo, lakini lilikuwa ni shambulio la pili la guruneti ndani ya wiki moja. Katika shambulio tofauti siku ya Jumapili, guruneti lilirushwa kwenye soko kubwa la kubadilisha pesa nchini, Sarai Shahzada, sio mbali na msikiti ulioshambuliwa. Hospitali ya dharura iliripoti kuwa shambulio hilo lilisababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 59 kujeruhiwa.


Wizara ya Mambo ya Ndani ya utawala wa Taliban ilidai kuwa shambulio hilo kwenye kitovu cha kubadilisha fedha lilikuwa ni kazi ya mwizi aliyejaribu kuiba sokoni. Wakati huo huo, sababu ya shambulio hilo dhidi ya msikiti wa Pul-e-Khisti katikati mwa mji wa Kabul bado haijafahamika.


Ghasia zimekuwa na utulivu wakati wa miezi ya baridi nchini, lakini sasa inaonekana kwamba idadi ya matukio inaongezeka huku hali ya hewa ikizidi kuwa ya joto.

Hata hivyo, Taliban wanasisitiza kuwa wameilinda nchi hiyo tangu kuchukua madaraka mwezi Agosti. Hata hivyo, maafisa wa Kimataifa na wachambuzi hawakubaliani na kauli hiyo, wakisema hatari ya kuzuka upya kwa wanamgambo bado ipo, na kundi la wanamgambo wa Islamic State limedai mashambulizi kadhaa makubwa.


Kundi la Islamic State la Mkoa wa Khorasan (ISKP, ISIS-K) hivi karibuni limeanzisha mashambulizi kadhaa huko Kabul na miji mingine. Mnamo Novemba, ISKP ilihusika na shambulio katika hospitali ya kijeshi huko Kabul na kusababisha vifo vya watu 19. Hapo awali, kundi hilo lilidai kuhusika na shambulio la kujitoa mhanga kwenye msikiti wa Shia huko Kandahar na kuua watu 60 mwezi Oktoba mwaka jana.


Mbali na tishio la kundi la Islamic State, makundi kadhaa yenye silaha, hususan yale yanayoundwa na shakhsia wanaopinga Taliban na vikosi vya usalama vya zamani vya serikali, pia yana changamoto ya usalama kwa watawala wapya wa Afghanistan.

0 Comments