BREAKING NEWS | Mwezi Haujaonekana, Tunakamilisha Thelathini Ramadhwaan. Iyd Itakuwa Jumatatu In Shaa Allaah


Hakuna taarifa zozote tulizozipata za kuonekana mwezi, baada ya juhudi kubwa za kufuatilia kwa karibu sana.

Na kwa kuifanyia kazi Hadiyth ifuatayo, tutakamilisha kesho Jumapili siku thelathini za Ramadhwaan na in Shaa Allaah Jumatatu, itakuwa ni siku ya kwanza ya Iyd.

Amesema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

صوموا لرؤيته وأفطروا لرؤيته فإن غم عليكم فأكملوا عدة شعبان ثلاثين (رواه البخاري)

((Fungeni kwa kuonekana (mwezi) na fungueni kwa kuonekana (mwezi) na kama umezingwa na wingu (usionekane) kamilisheni idadi (ya siku 30) za Sha'baan)) [Al-Bukhaariy]

0 Comments