Hilaal: Mwandamo Wa Mwezi Upi Sahihi Wa Kitaifa Au Kimataifa?

 Mwandamo Wa Mwezi Upi Sahihi Wa Kitaifa Au Kimataifa?


SWALI:

 

 Ni upi mwandamo sahihi wa mwezi kati ya mwezi wa kimataifa na kitaifa. 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Suala la mwandamo wa mwezi, ni suala lenye ikhtilaaf baina ya ‘Ulamaa.

 

Lakini mtazamo sahihi kwa nguvu za dalili zake, ni mwandamo wa popote pale unapoandama, Muislamu anapaswa kufunga na kufungua.

 

Hata hivyo, mas-alah haya kama tulivyotangulia kusema, ni yenye ikhtilaaf. Hakuna haja ya Waislamu kuzozana wala kugombana wala upande mmoja kukemea upande wa wengine.

 


Na Allaah Anajua zaidi


 

0 Comments