Viongozi wa bakwata na wakisiasa wahimiza watanzania kumuombea dua Rais wa Tanzania


Viongozi wa dini, Serikali na siasa nchini wamehimiza umuhimu wa kuendelea kumwombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwatumikia Watanzania kwa haki, usawa na uadilifu ili kuharakisha upatikanaji wa Maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ali, Naibu Waziri wa Mifugo Abdallah Ulega na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, walieleza hayo (jana) Alkhamis 28 Aprili 2022 waliposhiriki katika dua maalumu ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan iliyofanyika katika msikiti wa Mtoro Jijini Dar Es Saalam.


Dua hiyo iliambatana na mkesha wa ibada ya usiku maalumu wa "Lailatul al Qadir' ilihudhuriwa na viongozi na waumini mbalimbali wa dini ya Kiislamu nchini.

0 Comments